Searching...
Tuesday, May 6, 2014

Mirror kufanya collabo na Jose Chameleone’ asema" wimbo ni Mkalii"

Tuesday, May 06, 2014
10311248_293125287515901_1062200021_n


Muimbaji wa kampuni ya Endless Fame Films ya Wema Sepetu, Mirror amesema ni bahati kubwa kufanya collabo na msanii mkubwa Afrika Mashariki kama Jose Chameleone.
Wawili hao wamerekodi wimbo huo kwenye studio za AM Records chini ya producer Manecky Jumapili hii.
Mirror akiiambia Kikwetu Blog kuwa alifanikiwa kumpata Chameleone na kumshirikisha kwenye wimbo wake huo baada ya kukutanishwa na meneja wake (Mirror) waliyekutana na Chameleone kwenye tuzo za KTMA zilizofanyika Jumamosi kwenye ukumbi wa Mlimani City.
Amesema kesho yake alifanikiwa kumsikilizisha baadhi ya nyimbo zake na Chameleone akamshauri warekodi wimbo mpya kabisa.
“Kila kitu tumeshamaliza ni wimbo unasubiri kufanyiwa finishing tu uwe tayari,” amesema.
“ I am so happy kwanza ni ndoto yangu kwasababu Chameleone ni msanii mkubwa ambaye mimi nimeanza kumwangalia, kumsikiliza tokea niko mdogo so nilikuwa na dream kufanya naye kazi siku moja. Nafikiri na yeye pia amenikubali kama ni msanii mchanga ambaye ndio ninatoka sasa hivi. I am so proud kwanza kufanya nyimbo naye na nyimbo ni kali, watu wategemee kitu kikubwa sana,” amesema Mirror.
Share This:

0 comments:

Know us