CHUZI LIMECHACHUKA!
Na: Eno Bay Mtweve
Sura ya kwanza
Licha ya barua aliyomuandikia Hellea,Kunitisha Kuwa endapo nitakamilisha Mipango yangu ndoa na Lughano Lulamso, Maisha Yangu yange kuwa hatarini na kwamba yeye (hellena) hatalala usingizi hadi atakapo lipa kisasi, ayaharibu kabisa misha yangu lakini Tulifunga ndoa.
Harusi yetu ilikuwa kama jinamizi, ndoa ilifungwa asubuhi saa tatu kamili mwezi wa nane, haikuwa na shamrashamra bali tulikuwa watu wanne tu, yaani mimi nditi (ndiyo jina langu) machumba wangu lughano na wasimamizi wawili kama mashahidi. Tulikwenda kwa miguu ila wakati wa kurudi tuliahidiwa kuchukuliwa na binamu yake Lughano.Toka siku hiyo tukawa mume na mke.
Siku ya tatu Tangu tufunge ndoa, Lughano alionekana Kutochangamka kabisa kama mtu mwenye mawazo, sikumuuliza. Wakati wa kwenda Kulala Lughano alihuzunika kiasi cha kutoa Machozi! Baadae alinieleza kuwa Hellena alitaka Kujinyonga kwa Khanga bahati nzuri aliokolewa na akina mama walikuwa wakitafuta kuni msituni. Aliendelea kunieleza kuwa yeye amemuandikia barua kuwa hawezi Kuishi bila Lughano. Nilimuuliza kwa nini aliamua kumuacha mtu aliyempenda kiasi cha kutoa uhai wake?. Hakunijibu ila aliniinamisha kichwa chake kama mtu mwenye tatizo la kutoweza kuchanganua kati ya jambo jema na baya.
Hellena alikuwa Mchumba au niseme Mpenzi wa Lughano Takribani mwaka mmoja Jambo hili nilielewa Fika kwani uhusiano wao ulifahamika vyema kwa hapa Njombe. Sikujali sana kumnyang’anya tonge mdomoni kwani hata mimi nilichukuliwa na mchumba wangu siku za nyuma, hivyo niliona ni ulimwengu wa kudhulumiana “ujanja kupata” hellena alilazwa Hospitali ya Kibena Siku tatu, Baadae Nilipata habari kuwa binamu alifamfanyia Mpango wa kumuhamishia Dodoma.
Hellena alikuwa mwalimu na alifundisha shule ya msingi mabatini.Mimi nilikuwa ni muuguzi mkunga zahanati ya njombe mjini, na ndipo tulipoonana na kufahamiana na lughano, kwani katika shughuli zake za kazi yeye alitumia pikipiki kwa usafiri. Hiyo siku alipata ajali na kuumia goti hivyo alilazwa kwa wiki moja hakuwa mahututi na ndiyo maana tukafahamiana. Lughano alifanya kazi Katika Kampuni ya Mbegu Tanzania.
Maisha ya ndoa niliyaona mazuri, niliyazoea na kuyapenda halafu niliyaweza, japoluwa kulikuwa na mtafaruku mara chache. Tulijaliwa kupata watoto watatu, Midza, afisa na Safia wote walikuwa wa kike. Hali iliyomfanya mume wangu kunung’unika kwa kutokupata mtoto wa kiume. Niliamua niwe napata mimba mfululizo ili pengine nibahatishe mtoto wa kiume nifurahie nafsi yangu lakini hasa nimridhishe mume wangu. Miaka ilipita hatukupata mtoto si wa kiume wala wa kike.
‘’Nditii!” Aliniita Lughano siku moja ya Ijumaa “Bee!” Niliitika , “wanawake wengine bwana, Badala ya kuitika Bee Bwana wanaitika Bwee !!!” Utani ule ulinichoma kidogo ,na kujilaumu, kwa upungufu wangu wa kumudu mapenzi.Hata hivyo Lughano mwenyewe akiwa mpangwa wa Ludewa japo kuwa alinizidi mimi toka makete lakinialikuwa mbali sana, ingawa hakuwepo mwalimuwa kutufanyisha mtihani .Lughano alinipa barua niliisoma na nilielewa kuwa amepewa uhamisho ,kwa taratibu za kazi tulitakiwa kuhama wote, na tulihamia tanga.
Sura ya Pili
Maisha mjini Tanga yalikuwa ya kawaida ingawa wanapwani aghalabu walinibughudhi kwa kuniambia kuwa niwe na “mshikaji!” ili kuongeza mapato na starehe, Sikuweza kuelewa inakuwaje watu wafanye jambo hilo. Nilimpenda Lughano wangu niliamini kuwa nilimpata akiwa aghalin niilitosheka na kushiba penzi la baba Midza.
Tulikaa miaka sita pale Tanga, baadae tuling’amua kuwa siku zilikuwa zinaenda. Katika mambo kukamilisha ilikuwa ujenzi wa nyumba.Tulijadiliana na kuamua kuwa ilikuwa vyema kujenga sehemu za Njombe na hasa mjini Njombe,baada ya kulitafakari swala hili kwa marefu na mapana tulikubaliana mimi nirudi Njombe kwa shughuli za uhamisho na nikahamia hospitali ya serikali ya kibena, Karibu kabisa na mji wa Nombe Niliondoka na mtoto mmoja mdogo Sofia,huku nikiawaacha Midza na Afisa kukaa na baba yao.
Nilipofika Njombe sikupata njumba ya serikali kutokana na kuwa chache pia na udogo wa cheo changu, Ilinilazimu kupanga mjini Njombe Mtaa wa Ramadhani umabali wa kilometa tano hivi kufika kibena mahali nifanyiapo kazi. Kulikuwa na gari la hospitali lililotuhudumia kwani wengi tulikaa Njombe mjini, Hivyo suala la usafiri halikunipa shida sana.
ITAENDELEAAAA>>>>>>>>>
0 comments:
Post a Comment