MADA YA SABA: UANDISHI WA
BARUA |
Uandishi Wa Barua
Barua za kirafiki ambazo pia huitwa za kindugu huandikwa baina ya watu wa undugu au jamii moja. Katika mada hii utaweza kujifunza muundo wa uandishi wa barua ya kirafiki na jinsi ya kuandika barua ya kirafiki. Utaweza kutofautisha kati ya barua ya kirafiki na ile isiyokuwa ya kirafiki.
Barua za Kirafiki
Iwapo ni katika ndugu barua za kirafiki zaweza kuwa kwa watu kama: baba, mama, shangazi, mume, mke, mtoto, na kadhalika. Katika jamii waandikiwao barua za kirafiki ni kama jirani, rafiki, mpenzi, mwalimu, mwanafunzi, daktari, mgonjwa, na kadhalika.
Muundo wa Barua za Kirafiki
Mambo muhimu ya kuzingatia katika uandishi wa barua za kirafiki:
ANWANI kamili ya mwandishi, katika herufi hukaa juu upande wa kulia mwa karatasi.
TAREHE, chini ya anwani.
MTAJO wa heshima kwa anayeandikiwa, kama vile, mpendwa, mpenzi, na kadhalika, huandikwa kushoto, baada ya tarehe.
UTANGULIZI wa barua yenyewe ambao kwa desturi huwa ni salamu.
BARUA YENYEWE ambayo ndiyo kiini cha waraka.
SALAMU za kumalizia, pengine kwa jamaa na jamii.
HITIMISHO, katika aya, maalumu ambayo huwa, kwa mfano: 'Ni mimi baba yako akupendaye, ' na kadhalika.
SAHIHI ambayo si sharti wala muhimu sana.
JINA au MAJINA ya mwandishi, mwishoni.
Tazama mfano wa barua ya kirafiki:
Mfano 1
MUSOMA FISH PACK
S.L.P 4546
MUSOMA
23/5/2018
Mwanangu Nyamchele,
Ninafuraha kukujulisha kuwa nimepokea barua yako. Mambo yote uliyoyaeleza nimeyaelewa barabara. Huku nyumbani sote tu wazima na ni matumaini yetu kwamba afya yako
Tabia ya kulalamikia chakula ni mbaya. Tabia kama hii ikikomaa husababisha ulafi. Kumbuka hukwenda shuleni kula kama nguruwe. Huko shuleni nimekupeleka ili usome kwa bidii na ujifunze mengi. Usitamani kustarehe na kufikiria maakuli na anasa zingine za ulimwengu huu. Ondoa fikira za chakula akilini mwako na uache uzembe, eboo!
Hebu nikuonye kuhusu kuwapima na kuwachagua walimu. Walimu katika shule hiyo ni wabobezi na ndio maana nikakupeleka hapo. Wanajua mnayostahili kufundishwa. Huna ruhusa ya kusema eti walimu wengine ni wakali na hufundisha haraka haraka sana. Wewe unahitaji kutega sikio na kutii. Ukiwa makini na uwe na imani utayaelewa mambo unayofundishwa. Usisahau kuwa mchagua jembe si mkulima.
Mambo makubwa unayostahili kuyatilia bidii ni masomo yako. Muda wa miaka minne ni mfupi sana. Uonyeshe adabu njema kila wakati. Uwaonyeshe walimu wako taadhima na uwatii daima dawamu.
Jambo lililo kubwa katika shughuli yoyote ni uvumilivu. Ukivumilia utavuna matunda mabivu.Sitachoka kukusisitizia, 'Ukilima pantosha, utavuna pankwisha.' Fanya kila jitihada utimize mambo mengi iwezekanavyo kuanzia leo lakini usipapie chochote. Ndo ndo ndo hujaza
Mungu akubariki.Umwombe akusaidie katika kila jambo. Ujiepushe na maovu yoyo te Yale. Ukiwa na jambo usiwe na hofu kutuarifu mara moja. Mama yako amekusalimu sana. Amenikumbusha nikupashe hakuna refu lisilo na ncha. Kwaheri kwa sasa.
Ni mimi, baba yako akupendaye,
Magafu Malima
Barua ya Kikazi
ANWANI kamili ya mwandishi, katika herufi hukaa juu upande wa kulia mwa karatasi.
ANWANI kamili ya Mpelekewa, katika herufi hukaa juu upande wa kulia mwa karatasi.
TAREHE, chini ya anwani.
MTAJO wa heshima kwa anayeandikiwa, kama vile, mpendwa, mpenzi, na kadhalika, huandikwa kushoto, baada ya tarehe.
UTANGULIZI wa barua yenyewe ambao kwa desturi huwa ni salamu.
BARUA YENYEWE ambayo ndiyo kiini cha waraka.
Dhumuni la barua.
HITIMISHO, katika aya, maalumu ambayo huwa, kwa mfano: 'Ni mimi baba yako akupendaye, ' na kadhalika.
SAHIHI ambayo si sharti wala muhimu sana.
JINA au MAJINA ya mwandishi, mwishoni.
Mfano wa 2
MUSOMA FISH PACK
S.L.P 4546
MUSOMA
23/5/2018
Mkurugenzi Mkuu,
Shirika la Reli Tanzania,
S.L.P 76956,
DAR ES SALAAM.
Ndugu,
Yah: OMBI LA KAZI YA FUNDI UMEME
Mimi ni mwanamume mwenye umri wa miaka 30. Ninaomba Kazi ya Fundi Umeme kama ilivyotangazwa na Shirika la Reli Tanzania siku ya tarehe 28/06/2022 katika Tovuti, mitandao ya Kijamii na mbao za matangazo.
Nina Cheti cha Fundi Umeme nilichotunukiwa kutoka VETA mwaka 2021. Pia, nina uzoefu wa kufanya kazi na nimefanya kazi na Taasisi Ya 21st Century Holding LTD.
Kutokana na elimu yangu, uwezo wa kufanya kazi nilionao, uzoefu, pamoja na kuwa na sifa zinazotakiwa, ninaamini kuwa ninastahili kupata kazi hii. Endapo nitapata kazi hii ya Fundi Umeme, nitafanya kazi kwa bidii kama ilivyoelekezwa. Baadhi ya majukumu yangu ni: kutengeneza mifumo ya umeme, kuhakikisha vifaa vya umeme vinafanya kazi na kufuata maelekezo nitakayopangiwa.
Nipo tayari kwa usaili siku yoyote nitakayohitajika. Vilevile, ninatarajia majibu mazuri kutoka kwako na nimeambatanisha nakala ya vyeti vyangu kwa uthibitisho zaidi.
Wako mtiifu,
_________
MUSOMA FISH PACK
0 comments:
Post a Comment