MADA YA TANO: USIMULIZI |
UsİmuIİzİ ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengİ kuhusu tukİo fulanİ. Katika mada hİİ utajifunza juu ya taratİbu za usİmulİzİ wa matukİo kupİtİa njİa kuu mbİIİ za masİmulİzİ, yaanİ kwa njİa ya mdomo au kwa njİa ya maandİshİ. Pia utaweza kujifunza juu ya mbİnu mbalİmbalİ za usİmulİzİ.
UsİmuIİzİ wa Hadithi
UsİmuIİzİ hufanyika kwa njİa kuu mbİIİ yaanİ kwa njİa ya maandİshİ na kwa njİa ya masİmulİzİ ya mdomo. Kila njİa hutegemea namna msİmuIİajİ anavyoweza kuwasİlİana na msİkİIİzajİ. [kiwa msİmuIİajİ na msİkİIİzajİ hawakukarİbİana, njİa ambayo İtatumika ni İle ya maandİshİ. Kwa mfano kama utahİtajİ kumweleza mtu aliyembali kuhusu tukİo fulanİ la kusİsİmua utalazİmİka kutumİa maandİshİ, yaanİ utatumİa njİa ya kumwandİkİa barua. Lakinİ kama unamsİmulİa mtu ambaye yupo karibu nawe, utatumİa njİa ya mazungumzo ya ana kwa ana.
UsİmuIİzİ wa Habarİ
Taratİbu za UsİmuIİzİ wa Matukİo
UsİmuIİzİ wa matukİo dhamİra yake ni kumweleza mtu au watu tukİo ambalo wao hawakuIİshuhudİa. Hİvyo katika usİmulİzİ msİmulİajİ hutakİwa kutoa maelezo muhimu ambayo yatawawezesha watu hao kulielewa tukİo linaIosİmulİwa sawasawa na huyo anayeshuhudia. Mambo muhimu ya kutaja katika usİmulİzİ wa matukİo ni pamoja na haya yafuatayo:
1. Aİna ya tukİ0 — msİmulİajİ atatakiwa kubaİnİsha katika maelezo yake aina ya tukİo. Kwa mfano, kama ni hamsi, ubatİzo, ajalİ ya barabarani au mkutano.
2. Mahali pa tukİ0 — İli msİmuIİajİ aweze kuielewa habarİ İnayosİmuIİwa, ni lazİma kumwelewesha ni mahali gani tukİo hilo limetokea. Kwa mfano, kama ni mjİnİ İnafaa kutaja hata jina la mtaa.
3. Wakatİ — katika usİmulİzİ ni muhimu pia kutaja muda ambao tukİo limetendeka kama ni asubuhİ, mchana au jİonİ bila kusahau kutaja muda halisi yaanİ İlikuwa saa ngapİ.
4. Wahusİka wa tukİ0 — ni muhimu kutaja tukİo limehusisha watu gani, wİngİ wao, jinsİa yao, umrİ wao n.k.
5. Chanzo cha tukİ0 — kila tukİo lina chanzo chake hivyo ni muhimu kutajwa katika usİmulİzİ.
6. Atharİ za tukİ0 — atharİ za tukİo nazo ni shanİ zibaİnİshwe. Kama ni ajalİ, je watu wangapİ wameumia; wangapİ wamepoteza maisha n.k.
7. Hatima ya tukİo — msİmu[İajİ katika usİmulİzİ wake ni lazİma abaİnİshe baada ya tukİo kutokea na kushughulİkİwa hatima yake İlikuwaje. Kwa mfano, kama tukİo ni ajalİ ya barabarani hatima yake ınaweza 5 uwa majeruhİ kupelekwa hospİtaIİnİ na dereva alİyehusika kukamatwa.
Kwa hiyo misingİ hİİ ya usİmulİzİ hufanya usİmulİzİ wa tukİo kuwa na sehemu kuu tatu:
• UtanguIİzİ — sehemu hİİ huwa na maelezo tu ya utangulİzİ ambayo hulenga kuvuta hisia na umakİnİ wa msİkİIİzajİ au wasİkİlİzajİ. Kwa kawaİda utangulİzİ wa tukİo huwa ni maneno machache kİasİ yas İyozİdİ aya moJa.
• Kiini — kİİnİ cha usİmuIİzİ huelezea tukİo halisi kuanzİa chanzo chake, wahusika, muda, mahali na atharİ za tukİo.
tuhvle@qmail.c.m
• Mwisho — mwisho wa usimulizi ni matokeo yanayoonyesha matokeo ya mwisho ya tukio linalohusika, wakati mwingine matukio haya yanaweza kuambatana na maelezo ya msimuliaji kuhusu mtazamo au maoni yake binafsi juu ya tukio ambalo amesimulia.
Mbinu za usimulizi
Ili habari inayosimuliwa ipate
kueleweka vizuri, sharti msimuliaji ajue mbinu za kusimulia katika hali
inayovuta hisia za msikilizaji Wake
Baadhi ya mbinu hizo ni uigizi, utumizi wa lugha fasaha inayozingatia lafudhi sahihi ya Kiswahili.
Kwa upande wa uigizi msimuliaji
atatakiwa kuigiza mambo muhimu yanayohusiana na tukio ambalo anasimulia. Nayo
ni kama Vile milio, sauti na matendo.
Kwa upande wa usimulizi ambao unafanyika kwa njia ya maandishi, sharti usimulizi huo uwe na kichwa cha habari. Kichwa cha habari kinatakiwa kuandikwa kwa maneno yasiyozidi matano, yaliyoandile.va kwa herufi kubwa.
Kwa Vile usimulizi wa tukio huwa unahusu tukio lililopita, maelezo yake mengi huwa katika wakati uliopita.
0 comments:
Post a Comment