Ikiwa ni miezi nane imepita tangu afariki mkali wa mitindo huru, Albert Mangwea aka Ngwair, wimbo wake mpya alioupa jina la ‘Alma’ unatarajiwa kuachiwa rasmi February 14, 2014 ambayo ni siku maalum ya wapendanao (Valentine’s day).
Akiongea na tovuti ya DJMwanga.com, Muro ambaye ni moja kati ya wasimamizi wa kazi za Albert Mangwea ambaye anaisimamia project ya wimbo huo, amesema kuwa wimbo huo uliorekodiwa ndani ya studio za AM Records utaachiwa rasmi siku ya Valentine na kwamba anaendelea kuwasiliana na familia yake kuhusu mapato ya wimbo huo ambayo atapewa mama yake Ngwair.
“Yeye alitaka kuitoa ngoma hiyo siku ya Valentine mwaka jana, kwa hiyo na mimi nimeamua kuitoa siku hiyo hiyo. Niliongea na Familia Morogoro, na ntawapigia tena ili tuangalie tunachofanya kwa sababu kuna vitu vingi vya kuconsider, kuna mambo ya ringtones na nini na nataka nizungumze pia na makampuni ya simu. Kwa sababu kila alichotakiwa apate yeye (Ngwair) inabidi apate Mama yake.” Muro ameiambia tovuti ya DJMwanga.com.
Muro ameeleza kuwa wimbo huo wenye ujumbe wa mapenzi unazungumzia story ya kweli na ulikuwa maalum kwa mtu wa karibu wa marehemu Ngwair, “Kila kitu alichokuwa anakiimba kilikuwa cha ukweli, ni true story.”
January 16, 2013, Ngwair mwenyewe alitangaza kuwa ataachia wimbo huo siku ya Valentine (February 14, 2013) ambao alidai ni zawadi ya Valentine kwa fans wake na wimbo huo ulikuwa kwenye album yake iitwayo MIMI 3, lakini baadae aliahirisha na kuachia wimbo wa ‘Beef’ akiwa na TID.
Muro amesema kuwa kuna matatizo yalitokea wakati huo ambayo marehemu Ngwair hakupenda kuyazungumzia ambayo yalisababisha yeye kuahirisha kutoa wimbo huo.
Monday, February 3, 2014
Related Posts
Biashara | FTC KUENDELEA KUSIMAMIA MFUMO WA USHINDANI NA UDHIBITI WA MASOKO Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Uchumi toka Baraza la Ushindani (FTC) Bw. Nzinyangwa Mchany
Wapiga kura wapya milioni nne kuandikishwa kwa uchaguzi mkuu ujao Tanzania Tume ya Uchaguzi ya Taifa ya Tanzania (NEC) hivi karibuni itaanza zoezi la kuboresha uandi
Nchi Ya China Kuleta Watalii10,000 Kila mwaka Leo asubuhi (Jumapili, Oktoba 20, 2013) na Mwenyekiti wa Wakala wa kutoa huduma za usa
UTEUZI MPYA WA MAAJAJI,WAKUU WA WILAYA NA WAKURUGENZIWateule hao wataapishwa siku ya jumnne Tarehe 29 januari 2019
Members want draft constitution open debate 1st March 2014 NCCR-Mageuzi National Chairman James Mbatia Constituent Assembly
How to tell if your Android phone has the HummingBad malware Bad news: a malicious app has taken hold of about 10 million Android phones around the world
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment