Msanii wa muziki kutoka Zanzibar maarufu kwenye muziki wa mduara, AT, amesema kuna haja ya wasanii kutoka visiwani humo kupewa nafasi zaidi kuliko ilivyo sasa.
Amesema idadi ya wasanii kutoka Zanzibar wanaofanya vizuri Tanzania nzima ni chache ukilinganisha na wasanii kutoka bara licha ya kuwepo wasanii wengi wenye uwezo na kipaji cha muziki.
“Sisi tupo wachache kweli sio masihala hivyo tunahitaji kusaidiwa zaidi ili kuleta uwiano mzuri katika ufanisi wa kazi zetu na kukuza sanaa yetu,” alisema AT.
Miongoni mwa wasanii wa Zanzibar wanaofanya vizuri Tanzania nzima ni pamoja na Baby J, Berry White, Berry Black, Mzee Yusuf na wengine.
0 comments:
Post a Comment