Hiki ni kituo cha watoto wa chekechea ambacho kilianzishwa mwaka 2015, aprili, tarehe 14, na kilianza na wanafunzi 15 na mwaka ulio fuatia watoto walikuwa 20 na kati ya hao wengi wao wamejiunga moja kwa moja darasa la kwanza wakiwa na uwezo mkubwa sana.Na kwa miaka hiyo yote miwili wanafunzi walikuwa wakisoma kwa masaa matatu na nusu tuu,kuanzia saa 2:00 kamili asubuhi hadi saa 5:30 asubuhi.
Mwaka huu wa masomo 2017 kituo kimeweza kuanzisha mpango wa watoto kusoma kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa kumi na nusu 10:30 jioni pia hadi siku ya juma mosi ni siku ya shule.
DIRA
Kutoa elimu sahihi na malezi bora kwa watoto(wanafunzi) ili kutimiza malengo ya mtoto ,mzazi na jamii kwa ujumla.
Kutoa elimu sahihi na malezi bora kwa watoto(wanafunzi) ili kutimiza malengo ya mtoto ,mzazi na jamii kwa ujumla.
DHIMA
Kufundisha na kuwalea watoto kwa ustadi mkubwa na kuibua,kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto kwa kuwatengenezea mazingira sawia kwao.
Kufundisha na kuwalea watoto kwa ustadi mkubwa na kuibua,kukuza na kuendeleza vipaji vya watoto kwa kuwatengenezea mazingira sawia kwao.
Kuwafanya watoto wapende shule kwa kuwajengea ujasili wa kutatua matatizo kama kuepuka kufeli mitihani na woga kwa walimu n.k
WADAU /MARAFIKI WA NUECEKukamilisha malengo ya kiutekelezaji kituo kinashirikiana na
Wazazi wa watoto,
Serikali za mitaa, wajasiliamali wadogo na marafiki kama wewe.
SARE YA KITUO Traki nyekundu ,mzura wa kijani na kiatu chochote ila cha kamba vinavyo mfanya mtoto ang’are haswa na kuwa wa kipekee.
ANUANI
KIBENA SHULENI –NJOMBE, kwa mzee Bahari. SIMU: 0762088103
0718839483
0765496770
Barua pepe: nuecetz@gmail.com
HUDUMA NYINGINEZO.
Tunafundisha twisheni kwa wanafunzi wote wa shule za msingi na sekondari muda wote kwa gharama nafuu kabisa.mfano wakati wa jioni kuanzia saa nane( 8) mchana hadi saa kumi na mbili jioni (12) pia wakati wa rikizo na kwa pre- form one kuanzia mwezi wa nane au watisa na kuendelea.
Tunafundisha ENGLISH COURSE kwa wote
Tunatoa elimu ya ujasiliamali na ushauri pia KIINGEREZA kwa watoto na wakubwa siku ya jumapili kuanzia saa nane8 mchana hadi saa kumi jioni kwa shilingi mia 200 tu.
Tunafanya sherehe mbalimbali za watoto kama kusherekea siku zao za kuzaliwa (birthday) na mafanikio mengine.
KARIBUNI SANA
Kibao cha kituo kikiwa katika ukuta wa kibanda cha NGATA ukitokea stendi ya daladala.
Wanafunzi wa chekechea wakiwa katika michezo yao kituoni.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa kwenye mapumziko na hadithi mbalimbali
Wanafunzi mchanganyiko wakiwa darasani siku ya jumapili wakijifunza kiingereza kwa bei ileile ya sh.200/= tu
Baadhi ya PRE-FORM ONE baada ya kipindi wakiwa na mwalimu wao wa sayansi 2016
Katika matukio ya mhimu hatuko nyuma ....hii ni sherehe ya kuzaliwa (birthday) kwa wanafunzi wawili wa katikati Februali, 2017
Mwalimu wa michezo akiwa na wanafunzi wakiwa kwenye mchezo wa kubashiri..2015
Shukrani za dhati kwenu wote kwa jitihada mnazozifanya ili kujenga taifa letu.
KARIBUNI SANA NURU
SIMU: 0762088103
0718839483
0765496770
0 comments:
Post a Comment