MADA YA SITA: UANDISHI WA
INSHA |
Uandishi Wa Insha
Uandishi ni kitendo cha kupangilia maneno katika maandishi. Mada hii inazungumzia uandishi wa insha za wasifu kwa umahususi wake. Kabla ya kuanza uandishi utajifunza mambo muhimu yanayopaswa kuzingatiwa katika uandishi wa insha kwa ujumla, Utaelewa muundo wa insha na mwisho utajifunza juu ya dhana ya insha ya wasifu na namna inavyoandikwa na mwisho kabisa utaangalia mfano wa insha ya wasifu.
Insha za Wasifu
Insha ya wasifu ni ile ya kutoa maelezo juu ya jinsi mtu au kitu kilivyo, tabia, vitendo na mandhari (sura ya mahali jinsi panavyoonekana).
Mambo muhimu katika insha Ya wasifu ni: sura, rangi, umbo, vipimo, tabia, na kadhalika. Insha hizi zinaweza kuongelea kitu chochote kile, inaweza kuwa ni mnyama, mtu, Shule, nchi na kadhalika.
Hatua za Uandishi wa Insha
Kabla ya kuanza kuandika insha, ni muhimu sana uamue unataka kuandika juu ya nini. Inafaa uchague ile mada iliyo rahisi kwako kuweza kujieleza kikamilifu na kwa urahisi.
Kama unaandika insha za kufanyia mazoezi ni heri uchague mada zenye habari ambazo unazielewa. Iwapo hulijui au hulielewi jambo, ufanye uchunguzi kwanza. Ukisha kupata habari muhimu ndipo baadaye uandike insha yako kulingana na jinsi unavyoijua na jinsi unavyoikumbuka habari inayohusika.
Katika mtihani ni muhimu uyasome maagizo kwa makini. Kwa mfano, maayzo yanaweza kuwa: Chagua mojawapo ya habari zifuatazo kisha uandike insha isiyopungua kurasa mbili za karatasi za majibu.
Au:
Chagua mojawapo ya habari hizi kisha uandike insha ya maneno yasiyopungua 400.
Ni heri uandike insha nzuri ya kiwango kinachotakiwa kuliko ndefu (Zaidi ya maneno 400) ambayo haitakuwa na mambo muhimu hadi mwisho, na pengme yenye makosa na uchafu mwingi kupindukia. Ni muhimu ikumbukwe jinsi insha ilivyo ndefu, hasa katika mtihani, ndivyo idadi ya makosa inavyozidi kuongezeka.
Muundo wa Insha
Katika uandishi wa insha, muundo wake unakuwa na Vitu vifuatavyo:
Kichwa cha inshak kichwajcha insha juidokeza' kilé ålichokijadili katika insha yako. Kwa mfano: Madhara ya matumizi ya madawa ya kulevya n.k
2. Utangulizi; Mambo yaliyopo katika utangulizi ni pamoja na kutoa fasili ya maneno muhimu na kuelezea kwa muhtasari mambo ambayo utakwenda kuyajadili katika insha yako.
Kiini cha insha; katika kiini ndipo kuna maelezo ya kina juu ya kile unachokijadili katika insha yako, maelezo haya yanakuwa katika aya kadhaa kulingana na idadi ya hoja ulizonazo katika mjadala wako.
4. Hitimisho; hapa ndipo kuna muhtasari wa kile kilichojadiliwa katika kiini cha insha au inaweza kuwa ni msimamo juu ya kile kilichohadiliwa katika insha.
Zoezi 1 Tofautisha insha za kisanaa na zisizo za kisanaa.
0 comments:
Post a Comment