Taifa Stars iliifunga Cranes bao 1-0 Ijumaa (Machi 24), bao lililofungwa na Saimon Msuva dakika za lala salama na kutinga kwenye nafasi ya pili ya Kundi F wakiwa na pointi nne katika michezo mitatu waliyocheza.
Huo ulikuwa ushindi wao wa kwanza katika kampeni za kufuzu, na mwingine Jumanne utakamilisha hatima yao ikiwa Niger iliyo nafasi ya tatu itashindwa na viongozi Algeria katika mchezo mwingine. Itakuwa ni mara ya tatu kwa Tanzania kucheza fainali za AFCON, baada ya kufuzu mwaka 1980 na 2019.
Uganda nayo inazidi kuporomoka mkiani mwa msimamo ikiwa na pointi moja pekee na bado haijashinda katika mechi za kufuzu. Walifanya vyema dhidi ya Tanzania wiki iliyopita, na kuwaweka sawa kwa zaidi ya saa moja licha ya kuwa na mpira mdogo kuliko wapinzani wao. Licha ya kupoteza, meneja wa Cranes Milutin Sredojevic anaweza kubaki na XI sawa.
0 comments:
Post a Comment