Searching...
Friday, October 10, 2025

PROTECTOR Ya Simu HAIZUI KIOO KUPASUKA : ILA HUFANYA HIVI KWENYE SIMU YAKO

Friday, October 10, 2025



Protector ya simu ni Kioo kinacho ongezwa kwa kuwekwa  juu ya kioo cha simu kwa  la kupunguza  madhara ya kupasuka kwa kioo cha simu 

Kwanza zijue Aina Kuu za Screen Protector

​Kuna aina kuu mbili zinazopatikana sokoni:

1: ​Plastic Film (ya Plastiki): 

Faida: Ni nyembamba sana, nafuu, na huonekana vizuri kwenye simu.
Hata gharama zake ni nafuu sana

Hasara: Inatoa ulinzi mdogo sana. Inazuia mikwaruzo midogo (scratches) tu, lakini haitoi ulinzi mzuri dhidi ya kupasuka kwa kioo simu (cracks) simu inapoanguka. 
Simu nyingi mpya huja na hii imebandikwa kiwandani.

​2: Tempered Glass (Kioo Kigumu/Imara): 

Faida: Hii ndio chaguo bora zaidi kwa ulinzi wa jumla. Inahisi kama kioo halisi cha simu na inatoa ulinzi mzuri dhidi ya mikwaruzo na athari za kuanguka. Kioo cha protector hupasuka ili kufyonza mshtuko na kuzuia kioo halisi cha simu kupasuka.

Hasara: Ni nzito kidogo na gharama zaidi kuliko plastiki . Inaweza kuathiri unyeti (sensitivity) wa touchscreen au sensa (sensors) za simu kama haijatengenezwa vizuri.

3: ceramic   (ya Mpira 
Hii ni aina ya protector ambayo mara nyingi huwa na privacy au weusi ambao husaidia kuweka fagha maongezi ya mtu hasa jumbe za maandishi 

Faida : Hii huzuia kioo kukwaruzika tu na kuficha jumbe za maandishi endapi kuna mtu wa karibu anatizama chat au jumbe za maandishi hii ni bora kwa faragha y a mwenye simu. 

Hasara :  Hii hazui kupasuka kioo cha simu kabisa kwasababu inanesa, unaweza ona yenyewe nzima lakini kioo kikawa kimepasuka 

MUHIMU: Chagua Protector kutokana na simu yako kazi au mahitaji yako kwenye simu yako.. Kama unahitaji fargha chagua privacy Protector kama unahitaji kuzuia  kupasuka kwa kioo cha simu yako chagua Glass tempered protector 

Si uhakika sana glass protector itazuia kupasuka kwa simu yako : 

Kumbuka: Ili privacy Protector ifanye kazi tarajiwa Hakikisha umepunguza mwanga(brightness) wa simu yako 





Share This:
Next
This is the most recent post.
Older Post

0 comments:

Know us