Ndugu wa marehemu Frank Shoka aliyetuhumiwa kwa wizi wa kuku mwili wake ukisubiriwa kuja kuchukuliwa na polisi
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula aliyesimama kushoto amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
Polisi wakiuchukuwa mwili wa marehemu Frank
WAKATI jeshi la polisi Mkoani Mbeya likijitahidi kutoa elimu kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi, bado hali imezidi kushamiri baada watu wawili kuuawa kwa tuhuma za wizi wa mifugo.
Matukio hayo ywmetokea katika Wilaya za Kyela na Mbeya vijiji yakiwemo ya wizi wa kuku na ng’ombe jambo lililopelekea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa kuwaua bila kuwafikisha kwenye vyombo vya dola.
Katika Tukio la kwanza lililotokea katika kitongoji cha Katusi kijiji cha Mjere wilaya ya Mbeya vijijini wananchi wamemuua Frank William Shoka(30) kwa tuhuma za wizi wa kuku watatu mali ya Dismas Rashid(41)mkazi wa kijiji hicho.
Akizungumzia tukio hilo, Dismas Rashidi aliyeibiwa kuku hao alisema tukio hilo lilitokea Oktoba 20,mwaka huu na kuongeza kuwa marehemu alivunja banda la kuku majira ya usiku wa manane na kuchukua kuku watatu wakati yeye akiwa amekwenda kumuuguza mwanae katika kituo cha Afya Mjere ambako aliandikiwa sindano za masaa.
Alisema Baada ya kurudi nyumbani na kukuta kuku wake hawapo alianza kufuatilia na kumkuta marehemu akiwa na kuku hao katika kituo cha mabasi akitaka kuwasafirisha kwenda Mbeya,alipoulizwa juu ya kuku hao alikosa majibu wakati huo ikiwa ni saa kumi na moja alfajiri.
Alisema mtuhumiwa huyo baada ya kushindwa kutolea maelezo juu ya kuku hao wananchi walianza kumpiga kwa kutumia fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake hali iliyomfanya kupoteza maisha papo hapo mita chache kabla ya kufikishwa katika ofisi ya kijiji.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mjere, Mussa Tenson Mgula amesema alipata taarifa za tukio hilo kwa wananchi na alipofika alikuta mtuhumiwa ameshauawa hivyo alitoa taarifa kwa mtendaji wa kijiji hicho Evarist Benny ambaye alitoa taarifa kituo cha polisi Mbalizi majira ya saa mbili asubuhi ambapo Polisi walifika majira ya saa nane mchana na kuuchukua mwili wa marehemu.
Aidha Baada mwili wa marehemu kufanyiwa uchunguzi na Daktari mwili ulikabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwa taratibu za maziko,hata hivyo wakati wa tukio hilo mke wa marehemu aliyefahamika kwa jina la Mary Julius[30]alikuwa hayupo nyumbani akidai kuwa walikuwa wametengana.
Hata hivyo katika hali isiyokuwa ya kawaida wakati polisi wakisubiriwa mmoja kati ya kuku walioibwa alitaga yai moja na kuwaaacha wananchi katika hali ya mshangao.
Katika tukio la pili lililotokea kijiji cha Lupembe kata ya Katumba Songwe tarafa ya Unyakyusa wilaya ya Kyela Godfrey Mwakapalila mkazi wa kijiji cha Mpunguti aliuawa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake na kundi la wananchi walioamua kujichukulia sheria mkononi.
Chanzo cha mauaji hayo ni wizi wa ng’ombe mali ya Moto Mwakiange(36) mkulima na mkazi wa kijiji cha Muungano tukio lililotokea majira ya saa mbili asubuhi octoba,19 mwaka huu.
Kutokana na tukio hilo, Jeshi la polisi linamshikilia Moto Mwakiange kwa mahojiano zaidi wakati upelelezi ukiendelea wa kuwabaini watu waliohusika na mauaji,aidha mwili wa marehemu ulikabidhiwa kwa ndugu kwa ajili ya taratibu za mazishi.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya Diwani Athumani amethibitisha kutokea kwa matukio yote hayo na kutoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkoani na atahakikisha wale wote waliohusika na mauaji wanakamatwa ili kujibu tuhuma za mauaji.
Picha na Ezekia Kamanga
Mbeya yetu
0 comments:
Post a Comment