Mkutano wa siku mbili wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha (RCC) Umeelezwa kwamba Ziwa Manyara lipo hatarini kutoweka kabisa kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo uharibifu wa mazingira unaotokana na kilimo pembezoni mwa mito kama juhudi za makusudi hazichuliwi kutunza mazingira yanayozunguka maeneo ya mito mbalimbali inayoingia ziwani humo.
Hali hii imetokana na kuongezeka kwa shughuliza kibinadamu hususani za kiuchumi na kusababisha pia ziwa Manyara kujaa udongo na matope pamoja na uharibifu mkubwa wa mazingira.
Akiwasilisha mada kuhusu changamoto za uhifadhi katika hifadhi ya ziwa Manyara,Muikolojia katika hifadhi hiyo Bibi Christina Kiwanga amesema kukosana kwa utashi wa kisiasa ni changamoto kubwa katika kuliokoa ziwa hilo.
Bibi Kiwanga ametaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na kukosekana kwa mipango endelevu katika baadhi ya vijiji kuhusu umuhimu wa uhifadhi, sanjari na elimu.
Muikolojia huyo amewambia wajumbe wa kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Arusha kwamba shughuli za Biandamu hususani za kilimo na za kiuchumi zimechangia kwa kiwango kikubwa hifadhi hiyo kuwa katika hatari ya kutoweka.
Naye Meneja Ujirani Mwema makao makuu ya TANAPA, BWANA Ahmed Mbugi amesema umuhimu wa maeneo ya Mapito ya (SHOROBA) na mitawanyiko ya wanyama katika hifadhi amesema asilimia 80 ya Shooba zilizokuwepo miaka ya nyuma zimetoweka kabisa.
Amesisitiza kwamba ni lazima wananchi walinde uasilia wa mapito ya wanyama pori kutokana na umuhimu wa maeneo hayo
Mbungi amefafanua kwamba awali kulikuwa na Maeneo ya SHOROBA yenye ukubwa wa ekari 40,000 katika hifadhi za Arusha Kilimanjaro,manyara lakii maeeo haya yamepungua.
Aidha amesisitiza kwamba wanasiasa wanachangia kuhujumu maeneo haya ya uhifadhi kutokana na kukosekana kwa kuchukuwa maamuzi mazito ya kuyalinda maeneo hayo kwa kuogopa wapiga kura hali inayoleta changamoto mbalimbali pindi wanapotoa taarifa za kulinda maeneo hayo.
Pia ameeleza kwamba asilimia 70 ya mapato yanayotokna na uhifadhi yanatumika katika usajidia utekelezaji w amiradi ya kijamii ikiwemo ya afya,elimu, maji, na miradi ya barabara.
Amesema migongano baina ya wanyamapori na binadamu inachangiwa na binadamu kuingilia maeneo ya mapito ya wanyamapori hivyo kuwakosesha njia za kupita hali inayoharibu mazingira.
Amesisitiza kwamba hatua hii inasababisha kuathiri shughuli za utalii ambapo idadi ya watalii hupungua sanjari na shughuli za uchumi kuathirika Mbali na hali hii katika kipindi cha mwaka 1957/63 na 1987/`988 uoto wa asilimia hususani misitu ulipungua kwa asilimia 13.5 wakati maeneo ya kilimo yaliongezeka kwa asilimia 10.9.
Aidha maeneo ya ushorobo yaliyotumika kwa shughuli za kilimo kati ya mwaka 1997/98 yaliongezeka kati ya asilimia 8.35 hadi 11.41
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Lazaro Maasae yeye amesema kasi ya ziwa manyara kuendeleoa kujaa ugondo na matope ni ya kasi zaidi.
Mahmoud Ahmad Arusha
0 comments:
Post a Comment