Searching...
Thursday, August 25, 2022

BIASHARA YA PIRAMIDI | Unawekeza au Unawekezwa

Thursday, August 25, 2022

 

Mpango wa piramidi ni mtindo wa biashara wenye mchoro na usio endelevu unaotumiwa na walaghai kuwarubuni washiriki kwa ahadi za mapato ya haraka na ya kipekee katika muda mfupi. Huanza kwa wanachama wachache wa awali, wa ngazi za juu au washiriki kuajiri wanachama wapya ambao huwalipa gharama na ada za mapema ili kushiriki katika biashara.

sasa huu mfumo WAKITAPELI ulianza  miaka ya 1920s ambapo tapeli mmoja maarufu mwenye jina la Charles Ponzi alianza chukua pesa za watu na kuwaahidi kupata marejesho yenye faida zaidi ya asilimia 50%. Utapeli wa aina huu ulipewa jina la Ponzi Scheme kufatisha jina la tapeli wa kwanza kufanya huu utapeli.




Wanachama hao wapya nao huajiri wanachama wapya zaidi. Wao wenyewe hupokea ada zinazolipwa na ngazi hii inayofuata ya washiriki. Hata hivyo, sehemu ya ada hizi zinazofuata hutumwa kwa msururu kwa wanachama asili. Uandikishaji, malipo, na uongezaji ada hadi kupitia viwango mbalimbali vya piramidi unaendelea hadi hakuna mtu anayeachwa kuajiri. Wakati huo, mpango wa piramidi huanguka kwa ukosefu wa pesa zilizochukuliwa. Watu wengi wanaohusika hupoteza pesa zao


SASA hawa jamaa wanafanyaje ikifika kwenye kilele , Suluhisho lao  ni moja tu, wanafunga ofisi/platform zao na kukimbia na pesa zote walizoweka watu. Huku nyie mnabaki kujiuliza inakuaje mnashindwa kutoa tena pesa zenu.

juwa kuwa mchezo huu au mfumo huu  ni utapeli ambao tapeli huwalipi wawekezaji wa mwanzo pesa ya faida ambayo inatokana na wawekezaji wapya kwa kuwaahidi kupata faida kubwa ndani ya muda mfupi. ni ninyi kwa ninyi mnalipana na wa mwisho kuwekeza ndio alwaye 



Share This:

0 comments:

Know us