Searching...
Monday, March 27, 2023

MADA YA TATU; MATUMIZI YA KAMUSI [KISWAHILI FORM ONE]

Monday, March 27, 2023

 



Matumizi ya Kamusi 

Kamusi ni kitabu cha marejeo chenye msamiati uliokusan»va kutoka kwa wazungumzaji wa jamii fulani na kupangwa katika utaratibu maalumu, kisha kufafanuliwa kwa namna ambayo wasomaji wanaweza kuelewa. Au kamusi ni orodha ya maneno yaliyo katika karatasi au nakala tepe yaliyopangwa kialfabeti na kutolewa maana pamoja na maelezo mengine na kuhifadhiwa katika kitabu, santuri, simu, tarakilishi au katika mfumo wowote wa kielekroniki.

Kamusi huweza kuwa ya lugha moja, yaani orodha ya maneno pamoja na maelezo yake Yaki katika lugha moja Mfano 5

Mfano :

chatu,ni nyoka mkubwa na mnene

Kamusi nyingine huwa za lugha mbili yaani orodha ya maneno ipo katika lugha moja na maelezo ya maana ya maneno hayo yapo katika lugha nyingine.

mfano 6 chatu,npython

Kamusi ni hazina ya lugha inayohusika, kwani tofauti na vitabu vingine vya lugha, huwa na orodha ya maneno mbali mbali yanayotumiwa na wazungumzaji wa lugha ile pamoJa na maana zake. Japokuwa wingi wa maneno hutegemea ukubwa wa kamusi, kitabu hiki kina manufaa makubwa kwa mtumiaji wake kwani humpatia msamiati asioufahamu pamoja na maana zake au humpatia maana zaidi ya maneno anayoyafahamu. Taarifa zinazopatikana katika kamusi

Awali kamusi lilipoanza kutungwa zilikuwa ni orodha ya maneno magumu pamoJa na maana zake. Kamusi za siku hizi huwa na taarifa zaidi ya maana. Miongoni mwa taarifa ambazo kamusi huwa nazo ni:

*    tahajia za maneno mfano. Tasinifu Vs Tasnifu, Burangeti Vs Blanketi, Kula Vs Kura, mgme vs -engine  matamshi  sarufi ya lugha kama inavyojitokeza katika kila neno kama vile maumbo ya wingi wa nomino, vinyambuo vya neno kama vile chezesha, chezeka, che:ea, mchezo, mchezajin.k ambavyo vinatokana na kitenzi cheza

*    etimolojia ya neno (asili ya neno husika)  matumizi ya neno

Jinsi ya Kutumia Kamusi

Maneno yanayoingizwa katika kamusi hupangwa kwa utaratibu wa alfabeti. Maneno yanayoanza na herufi a, yote huwekwa chini ya hemfi A. Maneno yanayoanza na herufi fulani nayo hupangwa katika utaratibu wa alfabeti kwa kuzingatia herufi ya Pili, ya tatu, nne au tano ya neno kama mfano hapa chini unavyoonyesha. mfano 7

Mfano:ja, jabali, jabiri, jadhibika, jadi.

Maneno yote yanaanza na herufi [j]. herufi ya pili kwa maneno yote ni [a]. herufi ya tatti ni [b] na [dl. Kwa kuwa [b] hutangulia [dl katika mpangilio wa alfabeti maneno yenye [b] kabla ya yale yenye [dl. Kwa kuwa maneno yenye herufi [bl ni mawili itabidi tutazame herufi ya nne ya hya maneno ili tuchague litakaloorodheshwa mwanzo- Neno 'jabali' litaorodhewshwa kabla ya •jabiri' kwa kuwa [a] (herufi ya nne) ya 'jabali' hutangulia [i] ya 'jabiri' ambayo pia ni herufi ya nne. Kisha tunatazama maneno yenye [d] kama herufi ya tatu. Hapa tunaangalia pia herufi ya nne ili kubaini neno litakaloandikwa mwanzo kati ya •jadhibika' na 'jadi'. Kwa kuwa [hl hutangulia [il basi •jadhibika' huorodheshwa mwanzo ndipo lifuatiwe na 'jadi'

Kwa hiyo hivi ndivyo unavyopaswa kutafuta neno kwenye kamusi. Nenda kwenye herufi ya neno unalotafuta alafu litafute kwa kufuata mlolongo huo huo wa herufi ya kwanza kuorodheshwa.

Neno linaloorodheshwa kwenye kamusi ili lifafanuliwe linaitwakidahiz0.Kidahizo huandikiwa maelezo ya kukifafanua. Maelezo haya ni matamshi ya kidahizo, maana ya kidahizo, kategoria ya kisarufi, sentensi ya mfano wa matumizi ya kidahizo n.k. Kidahizo pamoja na maelezo yake ndio huitwakitomeo cha kamusi.


Mfano 

Kitomeo cha kamusi

Dhabihu (kidahizo)nm(kategoria ya neno) mahali pa kuchinjia wanyama (maana ya neno).

Taarifa Ziingizwazo katika Kamusi

Fafanua taarifa ziingizwazo katika kamusi

Maana la maneno

Kwa mfano:Dhabihunm mahali pa kuchinjia wanyama.

Kategoria za maneno

Kategoria za maneno kama Vile kielezi (ele), kitenzi (kt), kivumishi (kv), nomino (nm), kihisishi. Mifano ya matumizi

Kwa mfano, Waiziraeli huwapeleka koondo wao kwenye dhabihu kwa ajili ya ondoleo la dhambi. Lengo la kutoa mifano ni kumsaidia msomaji asiye fahamu vyema neno husika aelewe jinsi neno hilo linavyotumika.

Uingizaji wa nomino

Nomino nyingi katika lugha Ya kiswaili Zina maumbo Ya umoja na wingi.

Mfano:dumenmmamkopo;nm mi-

Viambishi ambatishi huwekwa kando Ya nomino kuashiria umbo la wingi la nomino.

Ngeli za nomino

Mfano:mkoponmmi- [u-/i-]

Kutafuta maana unayoitaka

Neno linaweza kuwa na maana moja au Zaidi ya moja. Maana inapokuwa moja mtumiaji kamusi hana tatizo kwani hiyo ndiyo atakayoipata na kuichukua. Lakini neno linapokuwa na maana Zaidi ya moja, mtumiaji kamusi hutatizika asijue ni ipi aichague. Ili kupata maana inayosadifu itafaa mtumiaji kamusi kutafuta maana ambayo inahusiana na muktadha wa neno linalotafutwa. Mfano:kifungonm vi-

1.      kitu cha kufungia

2.      kitu kinachotumiwa kufungia vazi kama Vile shati, gauni, suruali n.k

3.      adhabu ya mtu kuwekwa j ela kwa muda fulani

Iwapo mtumiaji aliona neno 'kifungo' kwa muktadha wa: "Juma alihukumiwa kifungo cha miaka kumi baada ya kupatikana na hatia ya kubaka.. Maana ya mukatadha huu itakuwa ni i le maana ya 3 kwa sababu ndiyo yenye kuhusiana na muktadha ambapo neno kifungo limetumika na wala Sio maana ya 1 wala ya 2.


*    Hupitishwa kwa njia ya mdomo

*    Ufanisi wa sanaa katika fasihi simulizi hutegemea uwezo wa msimulizi, au wahusika.

*    Masimulizi yake yanaweza kuathiriwa na mazingira, hisia na hali

*    Ni mali ya jamii. Hakuna mtu fulani anayemiliki sanaa katika fasihi simulizi.

*    Inaweza kubadilika kutoka kizazi hadi kizazi, au mazingira mbalimbali kwa sababu hutegemea kumbukumbu ya msimulizi.

*    Aghalabu huwa na funzo fulan

Dhima za Fasihi Simulizi

*    Kuburudisha - Hufurahisha na kuchangamsha hadhira

*    Kunasihi- kutolea mawaidha na kuonyesha mwelekeo unaotarajiwa katika jamii.

*    Kuelimisha watu kuhusu vitu mbalimbali hasa mazinglra yao

*    Kutambulisha jamii - jamii mbalimbali husifika kutokana na sanaa zao katika fasihi simulizi kama vile nyimbo.

*    Kuhifadhi na kudumisha utamaduni wa jamii

*    Kuunganisha watu huleta vatu pamoja

*    Kukuza lugha - fasihi huimarisha lugha kwa kuwa hutumia mbinu mbalimbali za lugha.

*    Kuliwaza - hutoa huzuni na kuleta matumaini.

*    Kupitisha muda - wakati mwingine fasihi simulizi hutumika kupitisha muda.

*    Fasihi simulizi ni chombo cha mawasiliano hususani kupitia ngomezi.

Dhana ya Fasihi Andishi

Fasihi Andishi ni aina ya sanaa ambayo hutumia maneno ya maandishi kupitisha ujumbe kwa hadhira.

Kuna tanzu kuu nne za Fasihi Andishi:

Hadithi Fupi — Hii ni kazi ya fasihi andishi yenye kisa kimoja na mhusika mkuu mmoja na maudhui yake sio changamani.

2. Riwaya —Ni kazi ya fasihi andishi yenye wahusika wengi na muundo changamani ni ndefu na maudhui yake ni mapana.

Tamthilia- ni kazi ya kisanaa yenye muundo wa kiugizikaji inayowasilishwa katika maandishi.

4. Mashairi - mashairi yakiwa yamechapishwa pia hutambulika kama fasihi andishi.

Sifa na Dhima za Fasihi Andishi

Sifa za Fasihi Andishi

*      Hupitishwa kwa njia ya maandishi

*      Ni mali ya mtu binafsi

*      Haiwezi kubadilishwa papo kwa papa

*      Hutumia mbinu za lugha na mbinu za sanaa katika uwasilishaji wake.

Dhima za Fasihi Andishi

*      Kukuza lugha

*      Kuhifadhi kazi ya sanaa katika maandishi  Kuburudisha

                                                                                                

*      Kuelimisha

*      Kukashifu tabia zisizoandamana na maadili ya jamii

*      Kuonya, kuelekeza, kunasihi

Tofauti kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi

Zifuatazo ni tofauti kati ya Fasihi Simulizi na Fasihi Andishi kama zilivyobainishwa katika jedwali hapa chini:

Kazi andishi ni 

1.mali ya mwandishi (na

2.Ni mali ya jamii.mchapi shaji)

Msimulizi anaweza kubadilisha sehemu

3.    Kitabu kilichoandikwa hakiwezi kubadilishwa Fulani

4.   Huhifadhiwa akilini            Huhifadhiwa vitabuni

5.    Kazi simulizi hubadilika na Wakati            

Kazi andishi haibadiliki na wakati

Huhitaji msimulizi na hadhira yake wawe Msomaji anaweza kusoma kitabu cha hadithi 6.

    mahali pamoja wakati wa masimulizi             peke yake, mahali popote, wakati wowote Ni lazima mwandishi na msomaji wawe na

7. Mtu yeyote anaweza kutunga na kusimulia uwezo wa kusoma

Hutumia wahusika changamano (wanyama,

8.  Hutumia wahusika wanadamu.

Share This:

0 comments:

Know us