Searching...
Friday, October 27, 2023

Doomsday SEHEMU AMBAPO MBEGU ZA Mazao yote ya ULIMWENGUNI HUWEKWA SALAMA

Friday, October 27, 2023
 BENKI YA MBEGU AINA ZOTE YA  IITWAYO DOOMSDAY

Ndani ya mlima wenye barafu kwenye kisiwa kilicho juu ya Mzingo wa Aktiki kati ya Norway na Ncha ya Kaskazini kuna rasilimali muhimu kwa mustakabali wa wanadamu. Sio makaa ya mawe, mafuta au madini ya thamani, lakini mbegu. Mamilioni ya chembe hizo ndogo za kahawia, kutoka zaidi ya aina 930,000 za mazao ya chakula, zimehifadhiwa katika Global Seed Vault kwenye Spitsbergen, sehemu ya visiwa vya Svalbard nchini Norway. Kimsingi ni sanduku kubwa la amana la usalama, linaloshikilia mkusanyiko mkubwa zaidi wa bioanuwai za kilimo ulimwenguni.
Share This:

0 comments:

Know us