Searching...
Sunday, November 19, 2023

MKURUGENZI WA OPENAI KURUDISHWA KAZINI

Sunday, November 19, 2023
OpenAI ni shirika la utafiti akili bandia  la Marekani (AI) linalojumuisha OpenAI, Inc.  Chat gpt, na zingine. 


Sasa Bodi ya OpenAI ipo kwenye mazungumzo kumrudisha Sam Altman kazini kama CEO.

Hii ni saa 24 baada ya bodi hiyo kukutana bila mwenyekiti wa bodi na kumuondoa Sam Altman kazini katika kampuni aliyoanzisha.

Ikiwa ni Saa 24 baadae tangu kuondolewa kwake kazini kuna mambo mengi yalitokea ambayo kwa kampuni isiyo ya faida huenda yakaharibu kabisa mwendo wa kampuni.

Tambua  kuwa Inasemekana Sam na Greg walishaanza kuzungumza na wawekezaji wengine juu ya uwezekano wa kufungua kampuni mpya.

Microsoft ni muwekezaji mkubwa zaidi wa OpenAI na wamesema hata baada ya Sam kuondoka wataendelea na OpenAI

Sasa chanzo kilicho karibu na Sam kilisema bodi imekubaliana na matakwa ya Sam ambayo ni kutengua uongozi wa Sasa na kwamba Sam atarudi yeye na mwenzake Greg Brockman na bodi iko tayari kujiuzulu.


Share This:

0 comments:

Know us