Movie inaanza hivii.. huko nyuma karne kadhaa zilizopita ambapo wahispania wanaenda huko America ya kusini katika msitu wa Amazon kutafuta kitu kinachoitwa "Tears of moon/machozi ya mwezi" ambao ni mti unaosimuliwa kuwa sehemu ya jani lake tu ina uwezo wa kuponya ugonjwa wowote au kuponya jeraha lolote na kuondoa laana yoyote.
basi baada ya mashujaa wengi wa kihispania kufa katika harakati hiyo ndipo kabila la wenyeji wa msitu huo linawatibu waathirika waliobakia kwa kutumia majani ya mti huo lakini wanakataa kuonesha eneo ulipo mti huo, ndipo wahispania wanaamua kuharibu kijiji hicho na hapo wanalaaniwa na chifu wa kijiji hicho na kugeuzwa kuwa mawe na miili iliyooza, na kulaaniwa kutokufa kamwe na kutokuwa na uwezo wa kuona njia ya kurudi kwao.
Baada ya karne kadhaa kupita ndipo mwanamama Dr Lily anagundua kitu kinachoitwa "Arrowhead/Kichwa cha mshale" na kuamini kuwa huo ndio ufunguo wa kuupata mti huo wenye uwezo wa kuponya
basi Dr Lily anaungana na nahodha mwenye uzoefu mkubwa aitwaye Frank ili ampeleke kuelekea kwenye msitu huo wa Amazon,wanatumia mashua kupitia njia ya mto hadi Amazon ili kuutafuta mti huo wa zamani ambao una nguvu na uwezo wa kuponya lakini wanakumbana na upinzani mkali kutoka kwa wajerumani ambao na wao wanaitaka "Arrowhead/kichwa cha mshale" ili kuupata mti huo. Utata wa kutosha unatokea hapa watu wanakufa sana na wanyeji wanashtukia hili na vita vikali sana vinatokea hapa.
0 comments:
Post a Comment