Mwanamume mmoja kutoka mkoani Njombe, Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania, alichukua hatua isiyo ya kawaida kwa kuanza kujijengea kaburi lake mwenyewe akiwa bado hai, ili kuondoa sintofahamu kuhusu hatima yake baada ya kufariki dunia.
Dkt. Anthony Mwandulami, ambaye pia ni mganga wa tiba asilia, alissema uamuzi huo ameufanya kwa hiari baada ya kutafakari maisha yake na mchango alioutoa kwa jamii. Kwa mujibu wake, alisema amekuwa akijenga kaburi hilo kwa takriban miaka minane sasa, akilifanyia maboresho hatua kwa hatua.
Hatua hiyo iliibua mjadala na mshangao miongoni mwa wakazi wa Njombe na hata katika maeneo mengine ya nchi, kwani si jambo la kawaida kwa mtu kujijengea kaburi lake mapema kabla ya kifo.
Akizungumza kuhusu sababu za kufanya hivyo, Mwandulami alisema kuwa ameona si vyema apotee tu bila kuwa na sehemu maalum itakayokumbusha familia na vizazi vijavyo kuhusu maisha na mchango wake.
Pia alieleza kuwa ameandaa kaburi hilo kwa ajili yake pamoja na wake zake watatu, jambo ambalo alisema wamekubaliana kwa pamoja kama familia.
Mke wake mkubwa, Damian, alisema wamepokea uamuzi huo kwa mtazamo chanya na wanaona ni maandalizi ya busara. Aliongeza kuwa wanaamini ni jambo la heshima na kumbukumbu kwa familia yao.
Kwa mujibu wa Mwandulami, mradi huo ulitarajiwa kugharimu takriban dola za Marekani 500,000 (zaidi ya shilingi bilioni moja za Kitanzania) hadi kukamilika kwake. Kiasi hicho kiliibua mjadala zaidi kutokana na viwango vya maisha vya eneo husika, ambapo fedha hizo ni kubwa kulinganisha na hali ya kiuchumi ya wananchi wengi wa kijijini humo.
Licha mipango mikubwa ya mwandulami, Ripoti zinasema mwandulami alifariki kabla ya kumalizika kwa ujenzi wa kaburi lake hilo la kifahari Miaka takribani mitatu iliyopita.
Maoni yako ni yapi katika hili.
Imeandikwa na
✍️ Zhuhura Abdullah
From facebook pge ya NZALI
0 comments:
Post a Comment